Published On: 25-10-2016 15:45:35

SAFARI YA KUHAMIA DODOMA

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya ustawishaji makao makuu Mhandisi Paskasi Muragili.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema lengo la serikali kuhamia Dodoma limepamba moto na litafanyika kwa awamu 6 katika kipindi hiki chan serikali ya awamu ya tano.

Majaliwa ameyasema hayo Bungeni Dodoma wakati akitoa hoja ya kuliahirisha Bunge hadi Novemba Mosi 2016 litakapo anza tena vikao vyake vya mkutano wa tano.

“Tayari imeandaliwa ratiba ya kuhamia Dodoma kwa awamu bila kuathiri bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 ambapo miundombinu iliyopo Dodoma inaruhusu serikali kuweza kuhamia Dodoma kuanzia sasa hadi mwaka 2020” Amesema Majaliwa

Amesema ratiba maalum ya kuhamia Dodoma imeandaliwa ambapo itaanza kuanzia mwezi huu wa Septemba 2016 hadi mwaka 2020 kama ifuatavyo.

Awamu ya kwanza ni kuanzia mwezi Septemba 2016 hadi Februari 2017 na itawahusu Waziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu wakuu wote na kila Wizara itatakiwa kuwahamisha watumishi wa idara moja au mbili na kuweka utaratibu wa kuhamisha watumishi wa idara nyingine.

Awamu ya pili ni kati ya mwezi Machi 2017 hadi Agosti 2017 ambapo katika kipindi hicho watendaji wa wizara mbalimbali kuweka watahusika na uhamaji ambapo wizara zitatakiwa kuweka vizuri bajeti zao ili kuendelea kuwahamisha wafanyakazi wake kwenda Dodoma.

Awamu ya tatu ni kuanzia mwezi Septemba 2017 na Februari 2018 ambapo wizara zitaendelea na zoezi la kuhamisha wafanyakazi wa idara zilizo katika wizara zao bila kuathiri bajeti iliyotengwa katika mwaka wa fedha 2016/17.

Awamu ya Nne kuanzia mwezi Machi 2018 na Agosti 2018 na Awamu ya tano ni Septemba 2018 hadi Februari 2020 ambapo katika vipindi hivyo wizara zitaendelea pia kuwahamisha wafanyakazi wake.

Awamu ya sita itakuwa ni kati ya Mwezi Machi 2020 hadi Juni 2020 ambapo Ofisi ya Rais ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watafika Dodoma.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amezishauri wizara zote kuanzisha mfumo wa kutunza kumbukumbu kwa njia ya kielektroniki kuliko kuhamia Dodoma na mafaili na Dodoma inatakiwa iwe ya kielekroniki.

Pamoja na hayo Waziri Mkuu amezikaribisha sekta binafsi na watu wanaotaka kujenga Dodoma kufanya hivyo ili kuweza kukidhi mahitaji ya watumishi na wageni watakaoingia Dodoma

CAPITAL DEVEROPMENT AUTHORTY

 Quick Links

Contact Us

Director General
P.O. BOX 913
Dodoma,Tanzania
Tel:   +255 262321569/+255 262324053
Fax:   +255 26 2322650
Email:   info@ cda.go.tz
Website:   www.cda.go.tz

Follow Us On: