Mkurugenzi Wa CDA Mhandisi Paskasi Muragili.

Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Paskasi Muragili, amewatoa hofu wakazi wa Dodoma kwa kusema kuwa ardhi mjini hapa itauzwa kwa bei ya kawaida ili watu wengi waweze kumiliki viwanja. Ameyasema hayo alipokuwa akijibu hoja za waandishi wa habari kuhusu kauli za wananchi kudai kuwa bei ya viwanja Dodoma itapanda kutokana na ujio wa Makao Makuu na kusababisha wananchi maskini kutoweza kumiliki viwanja hivyo. Muragili amesema kuwa viwanja hivyo havitapandishwa bei kwani kwa sasa Mamlaka inaua mita moja ya kiwanja cha makazi kwa Sh 5,500 hadi Sh 10,000 katika maeneo ambayo kitaalamu tunayaita ‘medium density’.“Viwanja kwa ajili ya uwekezaji mkubwa mita moja kwa Sh 13,300 na maeneo hayo kitaalamu tunayaita ‘low density’. Amesema pamoja na uwepo wa mahitaji makubwa, nasema ardhi ipo ya kutosha, yaani hata kama watakuja wananchi wote wa Dar es Salaam, watapata ardhi ya kutosha.“Narudia tena, ardhi ipo ya kutosha, hata kama watu watakuja baada ya miaka 30, wataipata kwa sababu hata Mwalimu Nyerere alipoamua Dodoma iwe makao makuu, alijua kuna ardhi ya kutosha kwa idadi yoyote ya watu,” Aidha Mkurugenzi Mkuu wa CDA Bw. askasi Muragili ametoa angalizo kwa wanaohitaji kununua viwanja mjini Dodoma na kusema watatakiwa kupitia CDA kwa kuwa ndiko vinakopatikana. “Viwanja tusinunue kienyeji, tufuate taratibu kwani najua watatokea wapigaji wa dili watakaowaumiza watu. Nawaombeni mje ofisini kwetu, kama mnataka viwanja mtapata tu kwa kufuata utaratibu,’’ alisema Amewaomba wananchi hasa wanaotoka nje ya Mkoa wa Dodoma kufuata sheria na taratibu za Mipango Miji taofauti na hapo Mamlaka haitasita kubomoa maeneo yamejengwa kiholela Akizungumia kuhusu suala la uwekeaji Dodoma Bw. Muragili amesema tayari Mamlaka imetenga maeneo ya uwekezaji la Njedengwa kwa ajili ya kujenga mahoteli makubwa na nyumba mbalimbali za kupanga. “Kuonyesha kwamba tulijipanga mapema katika eneo la uwekezaji, kule Ndejengwa miundombinu iliishafika mapema, kwani kuna maji, umeme pamoja na barabara za lami,” alisema Muragili.
CAPITAL DEVEROPMENT AUTHORTY

 Quick Links

Contact Us

Director General
P.O. BOX 913
Dodoma,Tanzania
Tel:   +255 262321569/+255 262324053
Fax:   +255 26 2322650
Email:   info@ cda.go.tz
Website:   www.cda.go.tz

Follow Us On: